May 17, 2016

Abiria Waanza Kulipa Nauli Mabasi ya DART

BIRIA leo wameanza kulipa nauli katika mabasi ya mwendo wa haraka (DART) yaliyoanza kufanya safari zake wiki iliyopita jijini Dar es Salaam baada ya siku zilizokuwa zimeongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, za kupanda bure kuisha.

Mtandao huu umefika katika kituo cha mabasi hayo kilichopo Morocco-Kinondoni jijini Dar na kukuta abiria wakikata tiketi huku wengine wakitoka katika safari zao licha ya baadhi ya abiria kuuambia mtaandao huu kuwa mashine za kukata tiketi zinakuwa hazifanyi kazi (kwa kupoteza netweki) ipasavyo na kusababisha foleni kwenye madirisha ya kukata tiketi.

Mwandishi wetu aliutafuta uongozi wa mradi huo wa mabasi (BRT) ili kuweza kuzungumzia kasoro hizo zilizotolewa na baadhi ya abiria lakini simu iliita bila kupokelewa
Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR