• Breaking News

  May 28, 2016

  Agizo la Magufuli Lamtumbua Muonyesha Filamu

  Kimenuka! Agizo la Rais John Magufuli la kuwataka watu kutotumia muda wa kazi kufanya starehe, limemtumbua kijana Mohamed Hamis (20) baada ya kukamatwa akiwa anaonyesha video kibandani, kazi iliyofanywa na Taasisi ya Haki Miliki (Cosota) hivi karibuni huko Temeke jijini Dar.

  Tukio hilo lilitokea Mtaa wa Azimio Kaskazini, ambapo maofisa wa Cosota waliingia mitaani kusaka watu wanaokiuka agizo hilo, sambamba na kuwatafuta watu wanaoonyesha filamu pasipo kuwa na leseni.

  Baada ya kukamatwa, kijana huyo alifikishwa kwa ofisi ya serikali ya mtaa ili wao waendelee na taratibu nyingine za kisheria dhidi yake.

  Akizungumza na gazeti hili, mwenyekiti wa mtaa huo, Misheli Manyamba alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai mtuhumiwa huyo atafikishwa polisi na baadaye mahakamani.
  “Ni kosa la kisheria kwa mtu yeyote kuonyesha filamu saa za kazi, anayekiuka agizo hilo ni lazima awajibishwe,” alisema mwenyekiti huyo.

  Naye ofisa wa Cosota aliyejitambulisha kwa jina moja la Suleman, alisema wao kazi yao ni kusimamia sheria za nchi na agizo la rais lazima liheshimiwa kwa kijana huyo kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku