• Breaking News

  May 25, 2016

  CCM Kuweni Makini 2020 Mnaweza Kupoteza Nchi

  Kama kuna kipindi upinzani utatoa upinzani wa khali ya juu katika historia ya vyama vingi basi ni kipindi hiki 2016--adi 2020,.
  CCM wanafanya kosa kubwa sana linaowaghalimu na litaendelea kuwaghalimu.

  CCM wanaamini kabisa nguvu JPM zimewapoteza kabisa wapinzani,hapana kwa kipindi cha miezi 3 iliyopita(febr --may) upepo umebadilika sana.

  Ndugu zangu CCM bila kuchukua hatua stahiki 2020 nchi inaondoka ,hawa wapinzani sio wakuupuzia ata kidogo.

  Tukumbuke hawa wapinzani in wajanja sana na wanajua sana Siasa za nchi hii,wakati nyota ya JPM IPO juu uku upepo wa wananchi ukimwendea vizuri,wapinzani walikuwa kimya kabisa hawakutaka kabisa kushindana na upepo huo,uku wakisubiri kujikwaa kwa mkubwa.

  Kusema ukweli JPM amefanya mambo mzuri kwa kiasi kikubwa,lakini kwa upande mwingine kuna masual mawili au matatu yameshusha credit za serikali.

  Mambo hayo ni...

  1. Ukosefu mkubwa sukari
  2. Kuonesha bunge live

  Ndugu zangu CCM kupuuzia mambo kama haya kwa kuyaona ni mambo madogo in kosa kubwa sana ,waswahili wanasema mzalau mwiba mguu huota tende.lshu ya sukari imeumiza sana wananchi wa chini tukumbuke hawa ndio wapiga kura.

  Kwa upande mwingine wapinzani wanatumia vizuri makosa ya serikali kujijenga na kujiimalisha,uku CCM ikiwa kimya.

  Naomba niseme kwa Mara ya kwanza tangu nikijue chama cha CCM yapata zaidi ya miaka 25 nashuhudi CCM ikiwa kimya kabisa katika mambo nyeti yanayotikisa taifa.

  Ndugu zangu CCM tuchange karata zetu vizuri,tulipata 8M, upinzani wakapata 6M kwenye uchaguzi uliopita ,tofauti sio kubwa alafu yule mzee wanamwitia mamvi amezinduka kwa kasi kubwa na kujiamini kwa kiasi kikubwa sana.

  Tusimpuuzie uyu mzee hatuwezi jua jinsi alivyojipanga na walionyuma yake kwa sasa.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku