• Breaking News

  May 26, 2016

  Dk Shein Amuwakilisha Magufuli Nchini Comoro

  Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein anaondoka leo jioni kwenda Muungano wa Visiwa vya Comoro kwa ziara ya siku mbili.

  Akiwa nchini humo Dk Shein atamuwakilisha Rais Dk John Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo, Azali Assoumani Boinakher.

  Kuapishwa kwa Boinakher kunafuatia ushindi wake alioupata katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika tarehe 10 Aprili 2016 na ule wa marudio katika kisiwa cha Anjouan uliofanyika tarehe 11 Mei, 2016.

  Sherehe hizo za kuapishwa Rais huyo mteule zitafanyika kesho katika kiwanja cha Mpira cha mjini Moroni na zinatarajiwa kuhudhuriwa viongozi mbalimbali kutoka nje ya nchi hiyo.

  Katika ziara hiyo Dk Shein amefuatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Bora , Issa Haji Ussi Gavu na Mshauri wa Rais Uhusiano wa Kimataifa, Uchumi na Uwekezaji Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa.  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku