May 9, 2016

Donald Trump Awakosha Wamerekani Adai Kodi na Mishahara Kuongezwa Akipata Urais

Bwenyenye Donald Trump,anayetarajiwa kugombea kiti cha urais kwa urais kwa chama cha Republican ameonesha yuko tayari kubadilisha msimamo wake, kuhusu maswala makuu mawili ya uchumi - kodi na kiwango cha chini cha mshahara.

Akihojiwa kwenye televisheni, alisema matajiri wanafaa kutozwa kodi zaidi, ambayo ni kinyume na sera ya muda mrefu ya chama cha Republican.

Mwaka jana alisema atawapunguzia kodi matajiri, Lakini sasa anasema, akichaguliwa kuwa rais, mipango yake itabadilika wakati wa majadiliano na baraza la Congress.

Aidha alisema kiwango cha chini cha mishahara kinafaa kuongezwa, lakini huo utakuwa uamuzi wa majimbo.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR