• Breaking News

  May 9, 2016

  Edward Lowasa ameiasa jamii ya watanzania kuwekeza katika Elimu

  WAZIRI Mkuu mstaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Edward Lowasa ameiasa jamii ya watanzania kuwekeza katika elimu hususani kwa mtoto wa kike katika kipindi hiki kigumu cha changamoto ya uhaba wa ajira hapa nchini na mahala pengi duniani.

  Lowasa anatoa nasaha hizo wakati wa kuwatunuku vyeti kwa wahitimu 70 wa kidato cha sita wa shule ya sekondari wasichana ya Irkisongo iliyopo Monduli shule ambayo yeye alisoma hapo kuanzia darasa la kwanza mwaka 1961.

  Lowasa amefafanua kuwa hivi sasa kuna ombwe la ukosefu wa ajira kwa vijana hivyo ni muhimu kwa jamii kuwekeza kwa mtoto wa kike zaidi kwani tafiti nyingi zinaonyesha ukimuelimisha mtoto wa kike umeisaidia jamii na kutoa wito kwa vijana wanaohitimu kidato cha sita hususani wa kike kujitahidi kuzishinda changamoto mbalimbali katika kipindi ambacho wanasubiria matokeo ili kutovuruga malengo yao ya kimaisha wanayoyatarajia.

  Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi mwalimu mkuu wa shule hiyo Happines Nyange amesema licha ya shule hiyo kuwa na mafanikio makubwa katika ufaulu wa wanafunzi wake lakini inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

  Shule hiyo ni miongoni mwa shule nne za sekondari za wasichana Wilayani Monduli ambazo Lowassa aliziasisi kwa lengo la kuwasaidia watoto wa kike kuweza kupata Elimu bora itakayowasaidia wao na jamii zao katika changamoto za kimaisha.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku