• Breaking News

  May 11, 2016

  Eliakim Maswi Atumbua Walimu Wawili Kiteto

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Eliakim Maswi amemvua madaraka mkuu wa shule ya sekondari Lesoit, Pekoslid Kambi ya Kata ya Lengatei kwa kudaiwa kufanya mapenzi na wanafunzi wa kidato cha pili na cha nne wa shule hiyo.

  Pia, Maswi amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Bosco Ndunguru kumsimamisha kazi ofisa elimu sekondari wa halmashauri hiyo, Rajab Chongowe kwa kumlinda mkuu huyo wa shule.

  Maswi amechukua uamuzi huo baada ya kutembelea shule hiyo kutokana na kitendo cha tume iliyoundwa na mkuu wa wilaya hiyo Kanali Samuel Nzoka kubaini kuwa mkuu huyo wa shule Kambi anafanya vitendo hivyo.

  Amesema Kanali Nzoka aliunda tume baada ya kupata malalamiko kutoka kwa walimu na wanafunzi juu ya tabia za mwalimu huyo kuwasumbua kila wakati kwa kuwataka kimapenzi baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku