• Breaking News

  May 14, 2016

  Haya Ndio Mabilioni ya Fedha Watakayopoteza Man United ikiwa Watafeli Kufuzu Champions League

  Ligi kuu ya England inamalizika wikiendi hii, bingwa tayari kashafahamika, timu 3 zinazoshuka daraja nazo zimefahamika. Wikiendi hii pamoja na ukamilishaji wa ratiba lakini kutakuwa na vita ya kuamua kati ya mbili za jiji la Manchester – ni ipi itapata nafasi ya kufuzu kucheza michuano ya ligi ya mabingwa wa ulaya baina ya United au City.

  Ikiwa Manchester City watashinda mchezo wao dhidi ya Swansea City basi haijalishi Man United watapata matokeo ya namna gani dhidi ya Bournemouth  – United wataikosa michuano ya ulaya mara ya pili ndani ya misimu mitatu mfululizo.


  Hii ni habari mbaya kwa mashabiki wa United lakini ni habari mbaya zaidi kwa mabosi wa MANCHESTER UNITED kwa sababu watapoteza kiasi cha angalau £30m (zaidi ya billioni 90 za madafu) kwa kuikosa michuano hiyo tajiri barani ulaya.


  CEO wa klabu hiyo Ed Woodward amewathibitishia wanahisa wa klabu hiyo  kwejye mkutano wa leo jioni lakini pia akawapa uhakika wa kupata faida.

  Lakini pia ikitokea United wakaikosa michuano hiyo msimu wa pili mfululizo, wadhamini wa jezi zao Adidas watapunguza asilimia 30 ya £750m za dili lao na klabu hiyo.


  Kikosi cha Louis van Gaal kilikuwa na nafasi ya kuipiku Man City jumanne iliyopita lakini wakashindwa kupata ushindi katika mchezo muhimu wa ligi dhidi ya West Ham United.

  Ripoti zinasema endapo tu United watashindwa kufuzu kucheza Champions League msimu ujao basi kibarua cha Van Gaal huenda kikaota nyasi na Jose Mourinho akatangazwa kumrithi pale Old Trafford.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku