May 8, 2016

Haya ni Mashetani Makubwa- Rais Magufuli

Rais John Pombe Magufuli leo akiwa Arusha amefunguka na kudai kuwa atalala sahani moja na wafanyabiashara wote ambao wanaficha sukari ili kuja kuiuza kwa bei ya juu kipindi cha mfungo.

Rais Magufuli ameeleza kuwa amepata taarifa kuwa Jijini Arusha yupo mfanyabiashara ambaye na yeye ameficha Sukari na kuahidi kushughulikia leo hii huku akieleza kuwa wafanyabiashara hao ni mashetani makubwa kwa vitendo vyao vya kuficha sukari ili wananchi wapate taabu.

"Kweli nitawakomesha hawa wasije kunilaumu, haiwezekani ukaficha sukari wakati viwanda vyetu vinatengeneza sukari, kuna mmoja yupo Arusha hapa naye nasikia ameficha sukari leo hii nitamshughulikia. Kuna mwingine alinunua sukari pale Kilombero zaidi ya tani elfu tatu akaficha, mwingine jana ameshikwa kule Tabata alikuwa ameficha zaidi ya tani elfu tano.

 Wanasubiri mwenzi mtukufu ili ndugu zetu waislamu wapate shida haya ni mashetani makubwa" amesema Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli amesema kuwa serikali yake haiwezi kushindwa kuleta sukari kwani wameamua kusomesha wanafunzi bure kuanzia shule ya mshingi mpaka sekondari kwa mabilioni ya pesa ije kushindwa sukari amedai kuwa watashindwa wenyewe na watalegea wenyewe.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR