• Breaking News

  May 13, 2016

  Heshima Aliyopewa Sumaye na Chadema Hakustahili na ni Matusi kwa Lowasa!

  Kila mtu anajua fika kabisa Lowasa amekuwa na mchango mkubwa sana tena sana kwenye mafanikio ya Chadema na UKAWA kwa ujumla...!

  Leo hii ukiwauliza wana chadema mchango wa Sumaye unao onekana hata kwa macho hawawezi kukuambia zaidi ya kusema alitoa hotuba!

  Lowasa amekuwa na mchango mkubwa sana kwa chadema kupata wabunge na hata kupata kura nyingi japo hazikuweza kuwapeleka ikulu lakini zitawapa ruzuku ambayo wataendelea kuitafuna!

  Sijui Mbowe na Lowasa wana makubaliano gani lakini kumnyima Lowasa ujumbe wa kamati kuu na kumpa Sumaye ni matusi kwa Lowasa ....!

  Wana jamvi kila mtu anajua fika kuwa Lowasa alijitoa sana kwa Chadema hadi alikuwa yuko tayari kufia jukwaani lakini awasaidie kupata wabunge na kura za kutosha!

  Kila mtu alitegemea kuwa ambaye angekuwa wa kwanza kupewa heshima ya kuwa mjumbe wa kamati kuu ya chadema ni Lowasa na si Sumaye....! Lowasa alipaswa kupewa hiyo heshima labda watwambie kuwa Lowasa ahitaji baraka za wajumbe wa kamati kuu ili kuwa mjumbe wa kamati kuu!

  Hakika watu wanasema tenda wema nenda zako nda ndicho anacho takiwa kufanya Lowasa maaana Chadema wameshindwa kutambua mchango wake...!

  Hivi Sumaye ameifanyia nini Chadema kustahili ujumbe wa kamati kuu zaidi ya Lowasa!

  Haya Matusi kwa Lowasa yataitafuna sana chadema tena sana nina hakika Familia ya Lowasa imeshangazwa sana na habari hizi....!

  Pole sana Mzee Lowasa!

  Karibuni wana jamvi!

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku