• Breaking News

  May 19, 2016

  HIVI UDART ndio nini? Sioni unafuu kabisa wa kupunguza foleni

  Sioni unafuu kabisa wa kupunguza foleni katika jiji la Dar, tabu iko pale pale , usumbufu ni mkubwa, watu mnabanana bora hata mabasi yetu ya Mbagala, unafuu wa usafiri uko wapi?uzingatiaji wa usalama wa afya za watu uko wapi? Watu mnapokea utaratibu mpya utafikiri umeanza miaka 50 ya Uhuru!

  Yaani plani hii imefeli kabisa pamoja na serikali kutumia mabillion ya pesa kwenye mradi huu ambao inaonekana kukosa tija! Watu tulijua labda tumepata usafiri ambao walao karaha za usafiri zitapungua lakini ndio kwanza matatizo matupu!Huu mradi ulianzishwaje bila kuzingatia idadi ya ongezeko la watu zinakopita barabara husika?

  Labda niulize msaada wa usafiri wa UDART kwa wakazi wa jiji la Dar ni upi? Hivi iko siku kuna mwanasiasa atasimama kujisifu juu ya mradi wa UDART?

  Hili lilikua Changa la macho hili! kwa lugha ya mtaani tuna sema "tumeliwa"

  By MAHANJU

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku