May 27, 2016

Jamaa Ang'atwa na Nyoka Uume Wake Alipokuwa Akijisaidia Chooni

ANG'ATWA UUME NA NYOKA THAILAND
Raia mmoja wa Thailand anaendelea kuuguza jeraha katika hospitali moja baada ya nyoka aina ya chatu kutokea ndani ya choo na kumng'ata uume wake.
Attaporn Boonmakchuay, ambaye alipoteza damu nyingi amesema kuwa nyoka hiyo alikuwa akimvuta baada ya yeye na mkewe kujaribu kumpiga.
Madaktari wanasema kuwa Bw Attaporn ambaye alipoteza damu nyingi anaendelea vyema na matibabu.
Baada ya nyoka huyo kutolewa katika choo hicho ambacho ilibidi kiharibiwe aliachiliwa na kuingia msituni. Kisa hicho kilitokea wakati ambapo Attaporn mwenye umri wa miaka 38 alielekea katika choo chake nyumbani kwake huko Chachoengsao,mashariki mwa Bangkok kabla ya kwenda kazini siku ya Jumatano.
Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR