• Breaking News

  May 7, 2016

  John Mnyika chagua moja kupinga ufisadi au kuzama kwenye tope la ufisadi kama Lissu.

  John Mnyika ni mbunge kijana ambaye alipikwa vema na Dr.Slaa.Alijulikana vema kwa kupinga ufisadi mafisadi.

  Maisha yake kisiasa yamegubikwa na simanzi kubwa iliyosababishwa na kubadili gia angani.Ikumbukwe tu Mnyika aliwahi kutoa tamko zito dhidi ya utawala wa Kikwete mwaka 2012 mbele ya media na nakala imo humu JF..iliyomtuhumu JK kumlinda Lowasa na sakata la Richmond na alieleza kuwa ana ushahidi wa uhusika wa Edward kwenye Richmond asilimia 100.

  Kwa sasa yupo kimya hataki kutupa vielelezo twende mahakamani.Ana maslahi gani?Amelipwa bei gani?

  Kwa sasa kageuka bubu bungeni na jimboni.Jipambanue upo upande gani?..Je upo 4U movement au chadema asili?..Katika makala yake katika gazeti la Raia Mwema tar.4/5/2016,Mwandishi Ben Saanane amenukuu utafiti uliofanyika huko kwa wazungu kuwa Tanzania inaongoza kwa unafiki,Je kwa "ububu" huu tutafsiri nini?

  Nakusihi amua moja,kupinga ufisadi au kuzama kwenye tope la ufisadi?

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku