• Breaking News

  May 21, 2016

  Jose Mourinho Kutangazwa Kuwa Kocha wa Man United leo? Taarifa hii hapa

  Manchester United wanategemea kumtangaza Jose Mourinho kuwa kocha wao mkuu leo, tangazo rasmi la usajili wa kocha huyo linategemewa kutolewa leo baada ya mchezo wa fainali ya FA Cup baina ya Manchester United vs Crystal Palace.

    Majadiliano ya mkataba wa miaka 3 yalifanyika baina ya CEO wa United Ed Woodward na wakala wa Mourinho, Jorge Mendes wiki kadhaa zilizopita; japokuwa kumekuwepo na sintofahamu kubwa juu ya usajili wa Mourinho kwenye bodi ya wakurugenzi wa Man United. Lakini baada ya majadiliano marefu maamuzi yakafikiwa kwamba haijalishi na matokeo yatakayotokea leo pale Wembley, utawala wa Van Gaal umefikia tamati.

  Mourinho alisaini makubaliano ya kabla ya mkataba wa kazi rasmi, ambao uliweka wazi kama kocha huyo hatopewa timu mwishoni mwa msimu basi angelipwa mamilioni ya fedha na Man United.

    Mourinho huenda akawa analipwa kiasi cha cha €15 million kwa msimu mmoja akiwa kocha Man Utd. Na pia Mourinho amepewa ahadi kupewa fungu la kubadili kikosi. Huku akifahamu fika mpinzani wake Pep Guardiola ambaye anajiunga na Man City nae amepewa fungu kubwa – na ikiwa hali itakuwa hivi basi jiji la Manchester busy sana kwenye soko la usajili.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku