May 12, 2016

Kamati Kuu ya CHADEMA, Itakutana Mjini Dodoma Katika Kikao Chake Kuanzia Mei 12-13

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari na umma wa Watanzania kuwa Kamati Kuu ya Chama itakutana Mjini Dodoma katika kikao chake cha kikatiba kuanzia Mei 12-13.

Kikao hicho, pamoja na masuala mengine, kitajadili kwa kina taarifa ya hali ya siasa nchini sambamba na mwenendo wa Serikali ya CCM ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ambayo imetimiza miezi 6 madarakani.

Aidha kikao hicho cha KK cha siku mbili, kitajadili na kupitisha Mpango Kazi wa Chama kwa mwaka huu (kutokana na Mpango Mkakati wa Chama wa miaka 5) kabla ya Sekretarieti kuanza utekelezaji, ambao utahusisha shughuli mbalimbali za chama ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa chama nchi nzima na kuendelea kuwatumikia wananchi.

Imetolewa leo Jumanne, Mei 10, 2016 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR