• Breaking News

  May 19, 2016

  Kwa hii kashfa ya Mbowe kugeuza CHADEMA kuwa kichaka cha Mafisadi, anapaswa kujiuzulu

  Siku zote viongozi na wafuasi wa upinzani wamekuwa wakipiga kelele sana kunapojitokeza tuhuma za ufisadi hasa kwa upande wa serikali na chama tawala. Siku zote wapinzani wamekuwa wakijiona wao ni malaika kwamba ni wasafi na hawakosei.

  Ila ukiangalia kwa jicho angavu, viongozi wa upinzani ni wasanii, wababaishaji na wapiga deal kimya kimya. Mpaka sasa, sioni uhalali wa Freeman Mbowe kusimama hadharani na kuinyooshea kidole serikali katika kashfa za ufisadi ambazo hazipo wazi ilhali yeye ndiye anawakumbatia mafisadi na amekuwa akiwapa madaraka makubwa makubwa ndani ya CHADEMA.

  Alianza na Lowasa ambaye amesemwa kwa zaidi ya miaka 8 kuwa ni fisadi. Ufisadi wa Lowasa si wa kificho na ndio uliomng'oa kwenye nafasi ya Uwaziri Mkuu mwaka 2008. Tangu wakati huo, Lowasa amekuwa akisemwa ama kuhusishwa kwenye matukio kadhaa ya ufisadi na Freeman Mbowe na Timu yake walitumia nafasi hiyo kuueleza umma juu ya ufisadi wa Lowasa. Kwa mtu mwenye akili timamu, aibu na dhamira njema ya kupambana na Ufisadi kivitendo, asingetegemea kuona Mbowe huyu huyu anasimama hadharani na kumtambulisha Lowasa kuwa ni mwanachama wa CHADEMA na kumpa dhamana kubwa ya kumteua kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya chama chake na UKAWA. Hii ni aibu kubwa ambayo ni lazima Freeman Mbowe abebe dhamana.

  Hata kabla kelele za kukemea uamuzi wa Mbowe kumpendekeza Fisadi Lowasa kuwa mgombea Urais hali iliyochangia anguko KUU la chama hicho na upinzani kwa ujumla hazijaisha, Freeman Mbowe huyu huyu anafanya maamuzi mengine ya GIZANI na ya aibu ya kumteua Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA licha ya mwanasiasa huyo kuhusika kwenye kashfa kadhaa ikiwemo kuuza nyumba za serikali na uuzwaji wa maeneo wazi (open space). Nafahamu kuwa CHADEMA hawana watu wenye maono kuongoza chama chao na ndo maana wanaokoteza tu hata makapi yaliyoachwa na CCM. Nafahamu kuwa mkakati wa Mbowe ni kuhakikisha kuwa Sumaye ndiye anapeperusha bendera ya CHADEMA kwenye uchaguzi Mkuu wa 2020. Ila kwa kashfa hii hakika Mbowe amepotoka

  Hata hivyo, ni vema wana CHADEMA na Watanzania kwa ujumla wakajiuliza, i wapi dhamira ya dhati ya Mbowe na chama chake kupambana na ufisadi na mafisadi? Inakuwaje mafisadi sasa wameifanya CHADEMA kuwa ni maficho yao na wamekuwa wakipata good shelter? Huu ujasiri wa Mbowe kuwakumbatia mafisadi na kuwapa vyeo anaupata wapi licha ya wafuasi wa chama hicho kupiga kelele ya kupinga maamuzi hayo na yeye amekuwa KIZIWI na KIPOFU?

  Kwa haya makosa ambayo Mbowe amefanya kwa kudhamiria, amepoteza hadhi ya kuwa kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Mbowe pia amepoteza hadhi ya kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA na kwa hali hiyo anapaswa kuachia ngazi mara moja ili kulinda hadhi ya upinzani na chama chake.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku