Natafakari kwanini kila nikisoma gazeti la Mwanahalisi naona mabaya tu ya serikali. Najiuliza kwani gazeti hili ni la chama fulani cha upinzani?

Kwanini wasiponde pabaya na kusifia mazuri ya serikali ya JPM? Enzi za JK waliponda ufisadi, sasa Magufuli anatumbua wanamponda yeye kulikoni?

Au wanatumiwa na watu wa nje kumdhoofisha Mh. Rais? Kwanini wasiwe kama gazeti la Jamhuri, mabaya yanaanikwa na mazuri pia?


Post a Comment

 
Top