• Breaking News

  May 13, 2016

  Lowasa Abariki Mbowe Kuwa Mgombea Pekee Uenyekiti..Kingunge Kukubali Ukamanda BAVICHA?

  Habari kutoka Mikocheni ni kuwa Mbowe kutopingwa uenyekiti CHADEMA kuelekea uchaguzi ndani ya Chama.Hii imetokana kile kilichosemwa "Mbowe umekuwa mwaminifu na msimamizi wa maagano tangu mwaka,2011"..Ikumbukwe ilishawahi kuripotiwa humu JF na baadhi ya magazeti kuwa Kuna "MOU" kati ya Chadema na EL kama plan "B" endapo angekatwa CCM na ndivyo ilivyokuwa.

  Huenda Kingunge kupokea kadi wakati wowote na kupewa ukamanda wa BAVICHA ambapo atapewa jukumu la kuunda itikadi ya chama kwa vijana ili kuendana na matakwa ya CHADEMA mpya.Hili ni suala linaloshughulikiwa na Mzee Lowasa mwenyewe hapo Mikocheni.

  Mabadiliko mapya yanakuja hasa kwenye Sekretariat ambapo majina makubwa yataondolewa ili kuleta damu mpya kutoka kundi la 4U ambao hasa ndio tegemeo kubwa la kubadilisha taswira ya chama.Kundi hili pia ndio litakuwa na nafasi kubwa kupewa nafasi ya kugombea udiwani,ubunge na uraisi siku za usoni. Hii itahusisha kukata majina ya baadhi ya makada wakongwe watakaojitokeza kuogombea nafasi za uwakilishi wa wananchi.

  Malalamiko ya kimya kimya yametokea lakini yamepuuzwa na mlango upo wazi kwa wabishi.

  Matokeo ya jambo hili yanatoa mwanya kwa makada marafiki wa Lowasa waliobaki CCM ambao hawafurahii maisha.Hasa wanaotuhumiwa na ufisadi na usaliti kujiunga na Chadema hasa pale uongozi utakapobadilishwa kuendana na matakwa na tabia zao.Na kuna wimbi kubwa pia la makada wa Chadema watakaotimka na huenda wakatua ACT.

  Kawaida ya JF kuweka kumbukumbu kuntu kama hizi.Uzi huu utabaki hapa kwa kumbukumbu ya vizazi vijavyo.Tujadili kwa ueledi ili kuleta tija kwenye Siasa zetu.

  Jamii Forums

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku