• Breaking News

  May 21, 2016

  Makonda: Nyama ya Vingunguti iuzwe Supermarket

  Halmashauri za Manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni zimeagizwa kujenga machinjio ya kisasa ili nyama inayotoka maeneo hayo iuzwe kwenye maduka makubwa (Supermarket).

  Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akifungua Machinjio ya Vingunguti yaliyopo Manispaa ya Ilala, yaliyofungwa zaidi ya mwezi mmoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) kupisha ukarabati wa miundombinu.

  Makonda alisema iwapo machinjio hayo yatajengwa na kufanya kazi kisasa, licha ya  kutoa nyama bora, watakuwa na uhakika wa kupata nyama itakayouzwa soko lolote ndani na nje ya nchi.

   Naibu Meya wa Ilala, Omary Kumbilamoto alisema kila kitu kipo sawa, changamoto zilizobaki watajitahidi kuzimaliza.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku