• Breaking News

  May 16, 2016

  Mambo 10 Muhimu ya Kufanya ili Kuendana na Kasi ya Mh. Magufuli

  Mambo 10 muhimu ya kufanya ili kuendana na kasi ya Mh. Magufuli
  1. Fanya kazi kwa malengo na ndani ya mda.
  2. Jifunze zaidi katika fani ya kazi yako....soma vitabu, angalia video, jifunze kutoka kwa wanaojua. Internet ina kila kitu. Punguza matumizi hovyo ya internet ya ku-socialize zaidi kuliko kujifunza.
  3. Epuka makosa ya kiuzembe yanayoweza kusababisha hasara kwenye maeneo ya kazi na maisha yako.
  4. Tumia mda vizuri (Effective time management). Mda ni mali.
  5. Epuka visingizio (excuses) na uongo. All excuses are equal as long as their results a zero or poor.
  6. Fanya kazi unayoiweza na kuipenda na siyo ili mradi kazi kwa sababu unapata mshahara.
  7. Epuka kuvumilia uzembe na wazembe kazini (Majipu)
  8. Kuwa kiongozi katika eneo lako la kazi (Self leadership)
  9. Jipime mchango wako kazini kama unaleta faida au hasara.
  10. Usipende kulalamika lalamika, kuwa sehemu ya majibu (Solutions).

  By Emillian Rwejuna

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku