• Breaking News

  May 26, 2016

  Mambo 15 ya kufanya kama serikali ya Magufuli inataka kuendeleza viwanda Tanzania

  Pengine sio yote yanafaa... lakini mengi yatasaidia

  1. Kwa miaka 5 serikali ielekeze nguvu kuinua viwanda vya bidhaa za chakula, hivyo...

  2. Serikali itoe ruzuku kwa uendelezwaji wa viwanda vya chakula kwa miaka 5, mathalani...

  3. Serikali iondoe kodi zote katika vifungashio vya bidhaa za chakula kwa miaka 5, kwa mfano...

  4. Makopo ya metal na plastiki, chupa za plastiki na glass, karatasi za nylon na za kawaida ihakikishwe zinazotengenezwa nchini au kuagizwa zipatikane kwa bei rahisi, kufanikisha hilo...

  5. Kwa miaka 5 serikali itoe ruzuku kwa viwanda vya kutengeneza vifungashio vya chakula, kwa mfano...

  6. Kwa miaka 5 gharama za umeme kwenye viwanda vya vifungashio vya chakula ziwe nusu ya gharama za kawaida, kisha...

  7. Serikali ihamasishe bidhaa zote za chakula, hasa vilivyo rahisi kusindika na kuwa packed visiuzwe bila kuwa packed, kwa mfano...

  8. Unga wa mahingi, Unga wa ngano, Mchele, Maharage/kunde, Nyama, Samaki, mayai na baadhi ya matunda viuzwe vikiwa packed, ili...

  9. Biashara yake iwe rasmi zaidi na uuzaji nje ya nchi uwe rahisi zaidi, na pia...

  10. Serikali iendeleze masoko ya ndani ya vyakula kwa kuyaboresha kimiundombinu na kuyarasimisha, tena...

  11. Serikali ihamasishe kufunguliwa na kusambaa kwa super markets, lakini pia bidhaa zote za chakula vilivyosindikwa na kufungwa nchini visilipishwe VAT kwa miaka 5, vile vile...

  12. Serikali ifungue mashamba makubwa ya mazao ya chakula kama mahindi, ngano, alizeti, maharage, mtama, miwa na mpunga, kwa kuyaendeleza hadi kiwango cha kuwa tayari kupanda mbegu (kusafisha pori, kutoa visiki na inapolazimu kuweka miundombinu ya umwagiliaji), kisha...

  13. Iyakodishe mashamba hayo kwa watu walioomba na kupatiwa mafunzo, huku wahitimu wa vyuo mbalimbali wakipewa kipaumbele, ambapo...

  14. Watakaokodisha mashamba hayo wataingia mikataba na wenye viwanda vya kusindika na kufungasha chakula ambao nao watakuwa na mikataba na wenye super na mini super markets, bila kusahau...

  15. Serikali iimarishe maabara za TFDA kuhakikisha vyakula vyote vinavyosindikwa na kufungashwa na viwanda vyetu, pia vinavyoagizwa nje ya nchi vinakuwa na ubora unaotakiwa.

  Naomba kuwasilisha

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku