• Breaking News

  May 21, 2016

  Comment ya Zitto Kabwe baada ya Rais Magufuli kumfuta kazi Charles Kitwanga

  Habari kubwa iliyoteka vyombo mbalimbali vya habari jana usiku ni habari ya Rais Magufuli Kumfuta kazi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga

  Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe ametumia ukurasa wake wa facebook kuandika mtazamo wake baada ya Rais Magufuli kufanya maamuzi hayo .

  “Uamuzi wa Rais kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani unatuma ujumbe mmoja – hataki mchezo. Rais amethibitisha kuwa anao uwezo wa kutumbua hata aliowateua. Ni maamuzi muhimu sana kwa Kiongozi wa aina yake. Wale vijana waliokuwa wanatumwa kumtetea wasimame kumtetea. Rais kaonyesha Uongozi ‘ no nonsense “

  1 comment:

  1. Hii ya kitwanga imetengenezwa
   ila completly set up 110%
   Mie binafsi ningemuona muheshimiwa anayo mahamuzi magumu,kama angemtimuwa kutokana na issues ya lugumi sio suala la pombe������

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku