• Breaking News

  May 13, 2016

  Mbunge Apasua Jipu.. Wanaokodishiwa Nyumba za Serikali Huzipangisha Kwa Watu wengine Kwa Bei za juu.

  Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolela (CUF) ameliambia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba watu wengi wanaokodishiwa nyumba za serikali huzipangisha kwa watu wengine tena kwa bei za juu.

  Mtolela ameyasema hayo alipokuwa akiuliza swali kwa Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambapo pamoja na mambo mengine Mbunge huyo ametaka kujua kama serikali ina fahamu kuhusiana na jambo hilo na hatua ambazo zimeshachukuliwa.

  Akijibu swali hilo Waziri mwenye dhamana ya nyumba na makazi nchini William Lukuvi amesema kwamba serikali inafahamu jambo hilo na mfano eneo la Samora jijini Dar es salaam na maeneo mengine watu wanazichukua na kuwapangishia watu wengine ambapo serikali itaanza kufanya uhakiki kuhusiana na jambo hilo.

  Aidha Waziri Lukuvi amesema kuwa utafiti uliofanyika mwaka 2010 ulibaini kwamba serikali itaweza kupata faida zaidi kama ikiboresha nyumba zake na kujenga nyingine na kupangisha kuliko kuuza.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku