• Breaking News

  May 27, 2016

  Mbunge wa Musoma Mjini, awatelekeza bila malipo vijana waliomlimia Shamba

  Vijana wapatao 100 waliokuwa wamepelekwa kwenye shamba la mbunge wa jimbo la musoma mjini vedastus mathayo lililoko kijiji cha nyabeu - bunda kwa lengo la kuwafundisha kilimo na kuwalipa mshahara wa tsh 300,000/= @ mwezi kama alivyokuwa akihaidi katika kampeni na mwisho wa mafunzo kila mmoja apewe tsh milioni tatu.

  Vijana hao wameshindwa kutekelezewa mahitaji yao licha ya kulima zaidi ya heka miamoja na sasa wameamua kutembea kwa miguu kutoka nyabeu umbali wa zaidi ya kilometa 15 na sasa wametia timu bunda mjini wanaomba msaada wa kufikishwa majumbani kwao Musoma mjini.

  Vijana hawa mpaka hivi sasa wako maeneo ya bomani bunda hawajala na wengine wanalia tu kutokana na maumivu ya kutembea umbali mrefu.

  Ombi lao kuu ni kuwawezesha kufika musoma

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku