• Breaking News

  May 3, 2016

  Mhe. Sumaye Asikitisha na Kuto Rushwa Bunge Live

  Tanzania leo imeungana na nchi nyingine Duniani kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, akisisitiza kuwa haki za binadamu, jamii zenye demokrasia na maendeleo endelevu vinategemea usambazaji.

  Akizungumzia hali ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini Tanzania Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Sumaye Vyombo vya Habari vina umuhimu mkubwa kwa serikali huku suala la kusitishwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge likionekana kuwanyima haki ya msingi ya kikatiba ya kupata habari wananchi.

  Mhe.Sumaye anasema katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasisitiza kulinda uhuru wa vyombo vya habari, na kuwaenzi wanahabari ambao huhatarisha maisha yao na wakati mwingine kupoteza maisha wakati wakifanya kazi yao na kusitisha kuwafikishia habari za moja kwa moja za Bunge ni kukiuka Katiba.

  Kwa Upande wake, Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Siasa nchini, George Maziku anasema katika kipindi cha muongo mmoja waandishi wapatao 800 wamepoteza maisha Duniani huku nchini Tanzania tangu mwaka 2012 waandishi wa habari watatu wamepoteza maisha katika mazingira tatanishi .

  Nao waandishi wa habari nchini wakizungumzia uhuru wa Vyombo vya Habari, wanasema bado sheria ya mwaka 1976 inampa mamlaka waziri kufungia gazeti endapo hatafurahishwa na habari itakayochapishwa, huku mazingira ya waandishi wenyewe bado sio rafiki.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku