• Breaking News

  May 11, 2016

  Mkuu wa Wilya Awasimamisha Watendaji Kwa Kuuza Makaburi

  WATUMISHI watatu wa Mji Mdogo wa Mirerani, wilayani Simanjiro Manyara, wamesimamishwa kazi na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mahmoud Kambona, wakidaiwa kuuza maeneo ya wazi likiwamo la makaburi.

  Watumishi hao waliosimamishwa kazi ni Kaimu Ofisa Mtendaji, Raphael Chao, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Endiamtu, Edmund Tibiita na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Naisinyai, Valentine Tesha (awali alikuwa Mirerani).

  Kambona akizungumza juzi alisema watumishi hao wanasimamishwa kwenye nafasi zao baada ya kulalamikiwa kuuza ardhi ikiwamo sehemu ya eneo la EPZA na makaburi.

  Alisema aliunda tume kuchunguza uuzwaji wa viwanja hivyo. Kambona alisema Chao alikuwa anakaimu nafasi ya Ofisa Mtendaji wa mji huo na ameondolewa kwenye nafasi hiyo kwa kushindwa kusimamia majukumu yake na kuzuia viwanja kuuzwa.

  Alisema kwa upande wake Tibiita alituhumiwa kusimamia uuzwaji wa baadhi ya viwanja vya eneo hilo na amesimamishwa kazi hadi uchunguzi wa jambo hilo utakapofanyika.

  “Huyu Tesha ambaye hivi sasa ni Ofisa Mtendaji wa Kata ya Naisinyai anasimamishwa kwenye nafasi hiyo kwa kutuhumiwa kuuza kiwanja akitumia muhuri wa kata ya Mirerani ilihali alishahamishwa,” alisema Kambona.

  Chao alipohojiwa alisema hawezi kuzungumza chochote na hawezi kupinga na uamuzi wa Mkuu wa Wilaya. Kwa upande wake Tesha alidai hayupo Naisinyai, bali yupo masomoni hivyo hawezi kuzungumza chochote.

  Kwa upande wake, Tibiita alisema anakubaliana na uamuzi wa Mkuu wa Wilaya hiyo wa kusimama kazi, ila anashukuru tume iliyoundwa ilithibitisha kuwa hana hatia na hahusiki kwa namna yoyote ile kuhusu uuzwaji holela wa viwanja hivyo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku