• Breaking News

  May 2, 2016

  Mlinzi wa Wizara ya Ujenzi Atupwa Jela Miaka Mitatu

  Ramadhani Kusena(48) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kushindwa kuzuia wizi usitokee katika Wizara ya Ujenzi, wakati akiwa mlinzi katika eneo hilo.

  Mshtakiwa huyo ambaye ni mkazi wa Temeke amehukumiwa kifungo hicho baada ya kushindwa kuzuia wizi usitokee katika wizara hiyo.

  Kusema alisababisha kiti na kompyuta moja viliibiwa katika chumba namba 303 kilichopo katika ofisi za wizara hiyo.

  Hakimu Mkazi wa Catherine Kioja alisema mahakama yake imemtia hatiani mshtakiwa huyo baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi wanne waliotoa mahakamani hapo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku