• Breaking News

  May 27, 2016

  Mourinho Asaini Mkataba wa Miaka Mitatu Manchester United

  Jose Mourinho amesaini mkataba na klabu ya Manchester United kuwa kocha mpya wa masheatani wekundu hao wa Jiji la Manchester.

  Mreno huyo aliondoka nyumbani kwake majira ya saa 11 na dakika 50 kwa saa za Afrika Mashariki, jana jioni, na kufanya mazungumzo ya mwisho na Makamu Mkuu Mtendaji wa Manchester United, Ed Woodward , mazungumzo yaliyofanyika, Hotelini London.

  Mourinho alirejea nyumbani baada ya mazungumzo ya saa moja na nusu, akiwa na makabrasha yake mkononi na chupa ya mvinyo mwekundu, mkataba ukiwa umeshakamilika kuwa kocha mpya wa Manchester United.


  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku