• Breaking News

  May 27, 2016

  Mrema Amshukia Maalim Seif ..Adai ni Mchochezi na Ingefaa Awe Ameshatiwa Ndani

  Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) ,Augustine Mrema,amedai Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Maalim Seif Sharif Hamad,alistahili awe amekwamatwa kwa kutoa Kauli za uchochezi.
  Mrema  ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu tangu ashindwe kiti cha Ubunge jimbo la Vunjo,Mkoani Kilimanjaro katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka jana,alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juu ya hali ya amani visiwani Zanzibar.

  Kauli ya Mrema imekuja huku Jeshi la polisi Zanzibar,likitarajia kumhoji Maalim Seif wakati wowote.
  Alida kuwa kitendo cha Maalim Seif kujitangazia matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana ni kinyume cha sheria.


  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku