• Breaking News

  May 20, 2016

  Msako unaendelea waliouwa watu Msikitini- Mwanza

  Jeshi la Polisi Jijini Mwanza tayari linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watu watatu katika msikiti mmoja kata ya Mkolani Jijini Mwanza.

  Watu hao watatu, akiwemo Imam, walifariki wakati wa shambulio hilo lililotekelezwa katika msikiti wa Rahman wakati wa swala ya usiku siku ya Jumatano.

  Kamanda wa Polisi Jijini Mwanza Ahmed Msangi amesema watu hao walitumia mapanga na majambia kufanya ukatili huo ambapo waliwauliza watu hao waliobakia msikitini baada ya swala ya usiku kwamba''Kwa nini nyiye mnaswali wakati wenzenu wameshikiliwa na polisi''?
  Aidha watu hao wanadaiwa kutozidi 15 ambao walijifunika nyuso zao huku wakishikilia bendera nyeusi yenye maandishi meupe.

  Aidha Kamanda Msangi amesema chanzo halisi cha mauaji hayo hakijabainika na uchunguzi unaendelea kuweza kupata watu zaidi waliohusika na tukio hilo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku