• Breaking News

  May 11, 2016

  Mtu na Mkewe Wafariki Dunia Baada ya Kula Chakula Chenye Sumu

  Watu watatu wamefariki dunia mkoani Kigoma katika matukio mawili tofauti likiwamo la mke na mme kula chakula kinachohofiwa kuwa na sumu na mtoto kufariki kwa ajali ya moto.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma SACP, Ferdinand Mtui amesema matukio hayo yalitokea Mei 8, mwaka huu.

  Amesema tukio la kwanza limetokea katika Kata ya Basanza ambapo Edson Kahenela (68) na mkwe Melisiana Petro (56) walikula chakula cha jioni wakaenda kulala na hawakuamka tena.

  Mtui amesema baada ya kuona hawaamki, mdogo wa marehemu aitwaye James Kahenela alipata mashaka na kugonga mlango lakini haukufunguliwa na hivyo kutoa taarifa kwa majirani ambao walivunja mlango na kukuta mke na mme wamekufa.

  Katika tukio la pili lililotokea maeneo ya mto Nsima Lugufu wilayani humo ilitokea ajali ya moto katika Nyumba ya Mayala Zalia na kusababisha kifo cha mtoto wake aitwaye Ligwa Mayala (1).

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku