Kwa kweli inasikitisha sana kuhusu mtaalamu aliye chora na kupitisha ramani ya barabara inayoanzia mwenge mpaka Tegeta. Wengi wa watumiaji tunapata taabu sana tunapotaka kuingia barabara za pembezoni.

Mara nyingi tumejikuta tukiwa katika hatari ya kugongwa kwa nyuma ya magari yetu kwa ukosefu wa maeneo ya kuwapisha wenzetu wanaotakiwa kwenda moja kwa moja.

Mfano mzuri ni pale Tangi Bovu kama unatoka mjini na unataka kuingia upande wa kulia yaani Ally Sykes road au anayetoka barabara hiyo na kutaka kuelekea Tegeta wote hao wanakuwa katika hatari ya kupata ajali.

Tunaomba mamlaka husika kabla ya kuipokea barabara hii watoe ushauri na maagizo ya kufanyiwa marekebisho sehemu zote hizo ili ionekane tuna wataalamu wanaojenga barabara za karne hii


Post a Comment

 
Top