• Breaking News

  May 6, 2016

  Mange Kimambi Hongera Sana Ujasiri wa Kuvalia Njuga Mambo Yenye Maslahi Kwa Taifa...

  Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza mwanadada jasiri asiyeogopa matokeo ya harakati anazofanya, ambazo nyingi zina maslahi kwa nchi yetu kwa ujumla wake.

  Nafahamu kwamba kuna watu wengi tu wanamchukia huyu dada kwa tabia yake ya kuweka kila kitu wazi bila kujali madhara yake katika jamii au kwake yeye na hata familia yake.

  Rejea madawa ya kulevya, na hata sasa alivyoamua kuacha kila kitu kikiwemo kile akipendacho UMBEA na kuweka maslahi ya Taifa mbele na zaidi akiungana na upinzani katika kuhakikisha kwamba Bunge linaonyeshwa live.

  Hili la Bunge kutokuwa live lilionekana kwa watu wengi kama jambo zuri lakini hawa watu hawakujua ni kwanini serikali ilianza harakati hizi za kuminya haki ya kupata habari ambayo ni haki ya kikatiba kwa watanzania wote.

  Hatahivyo, kati ya watu wachache waliojitolea kuungana na wabunge wa upinzani na wadau wengine ni huyu Mange Kimambi.

  Mange, nakupongeza sana kwa ujasiri wako wa kukosoa yale yanayoonekana kuwa na matokeo chanya kwa jamii yetu in a long-run.

  Hongera sana Mange na hongereni sana Wabunge wa Upinzani.

  Japo mimi ni mwana-CCM, lakini nilikuwa ni moja kati ya watu waliokerwa sana na hatua ya Serikali kuingilia Bunge na hivyo kulikuwa na hatari ya Bunge kama Muhimili muhimu wa kuisaidia serikali katika kuendesha nchi kukosa nguvu na kuwa sehemu ya serikali.

  Jambo hilo likitokea, basi tulipokuwa tunaelekea ni kubaya kuliko tulipotokea.

  NARUDIA TENA, HONGERA SANA DADA MANGE KIMAMBI NA MUNGU AZIDI KUKUPIGANIA WEWE NA FAMILIA YAKO.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku