EgyptAir Flight 804 imepoteza mawasiliano ikiwa angani kutokea Paris Ufaransa kwenda Cairo Misri ambako ilitakiwa kutua saa kadhaa zilizopita kwa mujibu wa CNN lakini ikapoteza mawasiliano ikiwa tayari imeingia kwenye anga ya Misri.

Shirika hilo la ndege limethibitisha kwa kusema ilikua na abiria 56 na Wafanyakazi 10 ndani yake ambapo mpaka sasa msako umeshaanza kujua ilipo ndege hii ambayo ilipotea ghafla na kutoonekana kwenye Radar.

Ndege hii imepotea ikiwa kwenye umbali wa futi elfu 37 hewani, rubani wa ndege hiyo anao uzoefu wa kurusha ndege kwa saa 6000 huku msaidizi wake akiwa na uzoefu wa saa 4000


Post a Comment

 
Top