• Breaking News

  May 8, 2016

  Ndugai Apinga Watumishi Kuishia Kusimamishwa

  Spika Job Ndugai ametaka operesheni ya kushughulikia wazembe kazini iongezwe nguvu kwa kuunda sheria ya kuwatimua badala ya kuwasimamisha kazi kwa uchunguzi kama inavyofanyika sasa.

  Ndugai, ambaye ni kiongozi wa Bunge ambalo kazi yake ni kutunga sheria, alimuomba Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kumshauri Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kupeleka haraka bungeni muswada wa sheria itakayoruhusu watumishi wazembe wafukuzwe badala ya kusimamishwa kazi.

  Kauli ya Ndugai imekuja wakati Taifa likiwa kwenye mjadala kuhusu vitendo vinavyofanywa na viongozi wa Serikali vya kusimamisha watu kazi kwa kutangaza tuhuma zao kwenye mikutano ya hadhara na baadaye kuagiza uchunguzi ufanyike jambo ambalo wadau wa utawala bora na wanaharakati wanasema ni ukiukwaji wa sheria.

  Wadau hao wanasema watuhumiwa hawana budi kuchunguzwa kwanza kabla ya kutangazwa hadharani kuwa wana makosa, wakisema kutofanya hivyo ni kushawishi uchunguzi ufanyike kwa lengo la kuwatia hatiani badala ya kutafuta ukweli.

  Akizungumza kwenye kikao cha Makamu wa Rais na viongozi wa CCM mkoani Dodoma jana, Ndugai alisema sheria iliyotungwa ya watumishi wa umma si nzuri kwa kuwa inatumika kuwalinda hata wasiostahili kuwapo kazini kutokana na uzembe na ubadhirifu.

  “Sheria za kuwalinda watumishi hazifai, ni bora mkamshauri AG azilete zote bungeni kwa wakati mmoja tuzipitishe ili wazembe na wabadhirifu wafukuzwe si kusimamishwa,” alisema Ndugai.

  Alisema wakati mwingine amekuwa akishangaa kuona jinsi watu wanavyoharibu, lakini wakitaka kufukuzwa sheria inakuwa kikwazo na kulifanya Taifa kuingia katika hasara.

  Alisema sheria hizo zikipelekwa bungeni atazisimamia zipitishwe haraka zote kwa wakati mmoja ili kuondokana na dharau inayofanywa na baadhi ya watumishi wasiokuwa na huruma na taifa lao.

  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa alikiri kuwa nafasi ya chama katika ngazi ya chini ni ndogo kwani CCM inaonekana kuanzia ngazi ya wilaya hadi Taifa pekee.

  Kimbisa aliwataka madiwani na watumishi wengine kutomwangusha Rais na badala yake waache kuwanyenyekea watumishi wa Serikali, bali wawawajibishe pale inapobid

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku