May 6, 2016

Rais Dr. Magufuli Amsimamisha Kazi Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mji wa Babati Ndugu Omari Mkombole

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Babati Ndugu Omari Mkombole. Omari Mkombole alihamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati na kupelekwa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma mwishoni mwa mwaka jana.

Rais ameyasema hayo leo mchana katika mji wa Babati karibu na Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mji wa Babati aliposimamishwa kusikiliza kero zao wakati akitokea Dodoma kuelekea Arusha.

Rais aliyasema hayo alipoulizwa na mwananchi mmoja kero za ardhi zinazowakabili hasa zinazohusu Shamba la Makatanini. Rais alimjibu mwananchi kwamba taarifa zote za ardhi anazo na anazishughulikia. Rais akasema amemsimamisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati kwa tuhuma zinazohusu uuzaji wa ovyo wa shamba la Makatanini.

Kusimamishwa huku kumekuja baada ya Tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Kocha Joel Bendera na kugundua kero nyingi na ubadhirifu katika mradi wa kuuza viwanja katika shamba la Makatanini na sekta nyingine zinazosimamiwa na Halmashauri ya Mji wa Babati

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR