• Breaking News

  May 13, 2016

  Rais Magufuli Akerwa Kudanganywa Uwanja wa Ndege

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewasili nchini akitokea Uganda ambapo alishiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni.

  Rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ambapo ametembelea eneo la kukagua mizigo pamoja na abiria na kukuta mashine haifanyi kazi kwa muda mrefu.

  Kufuatia hali hiyo Rais Magufuli amehitaji sababu za msingi za kutofanya kazi kwa mashine hizo ambapo Maafisa wa uwanja huo walionekana kutoa maelezo ambayo yametofautiana jambo mbalolimemfanya Rais kuagiza vyombo vya dola na wizara husika kuchukua hatua mara moja.

  ''Unajua mimi sipendi kudanganywa ni vizuri uzungumze ukweli tu, kwa nini nimeanzia hapa huwezi kujiuliza? Eee sasa sipendi kudanganywa, ukinidanganya nitachukia sasa hivi, wewe umenidanganya kwamba hiyo ndiyo mbovu, na hii ndiyo nzima, nikawaambia muiwashe hiyo nzima, akaja huyu mwenzako amezungumza ukweli kabisa akasema hii mbovu kwa miezi miwili'' Rais amewahoji maafisa hao wa uwanja wa ndege.

  ''Kwa hiyo mizigo inayoingia humu huwa hamuikagui kwa namna yoyote, kwa hiyo nikiamua kuja na madawa yangu ya kulevya, nikaja na dhahabu zangu, nikaja na almasi zangu na meno ya tembo kwa kutumia hizi ndege ndogo ndogo napita tuu''- Rais Magufuli amezidi kuwabana maafisa hao.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku