• Breaking News

  May 10, 2016

  Rais Magufuli awataja wafanyabiashara wanaosumbua kwenye sukari

  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli ametangaza kupambana na wafanyabiashara wanaohodhi biashara ya sukari ambao hawazidi hata 10.

  Akizungumza kwenye ufunguzi wa majengo ya NSSF na PPF jijini Arusha jana, rais Magufuli amesema wafanyabiashara hao ndiyo walishiriki kuviuwa viwanda na kujitajirisha binafsi.

  “Wafanyabiashara hawa walinunua viwanda vya NMC wakafungua mashine na kwenda kuuza Msumbiji na wakisimama utawasikia CCM oyee,” aliongeza.

  Rais Magufuli amesema atapambana na wafanyabiashara hao bila ya kujali ni wafuasi wa CCM, Chadema au CUF atalala nao mbele kwa mbele.

  Aidha Magufuli aliendelea kusema, “Utakuta Watanzania tunaendeshwa na wafanyabiashara kati ya watano au kumi tu, ukienda kwenye sukari ni hao hao, walioua viwanda ni haohao, nawahakikishia nitalala nao mbele hadi mwisho.”


  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku