May 27, 2016

Rais Magufuli Kujaza Vijana Serikalini, Amegudua Haya Kwa Vijana..

Moja ya stori kubwa ni hii ya gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Magufuli kujaza vijana Serikalini‘ Gazeti hili limeripoti kuwa Magufuli amesema kuanzia sasa wateule wengi wa Serikali watakuwa vijana kwa kuwa amegundua wengi hawapendi rushwa.

Gazeti hilo limeongeza kauli ya Rais Magufuli kuwa anafahamu kwamba vijana hawapendwi lakini amegundua ndio wachapakazi ambao watasaidia kulipeleka Taifa katika maendeleo anayoyatamani kwani aliowaweka tayari ameshaanza kuona matunda ya kazi zao.

Rais Magufuli aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa makandarasi wa mikoa ya Dar es salaa, Mbeya na Dodoma.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

1 comment:

  1. Tuweke baba tupooo tuweke tufanya kazi....

    ReplyDelete

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR