• Breaking News

  May 12, 2016

  Rais Magufuli: Wasumbufu wa Sukari Hawazidi 10 Tanzania, Nitapambana Nao

  Rais John Magufuli ametangaza kupambana na wafanyabiashara wasiozidi 10 waliohodhi biashara ya sukari, akisema ndiyo wameshiriki kuua viwanda na kujitajirisha.

  "Wafanyabiashara hawa walinunua viwanda vya NMC wakafungua mashine na kwenda kuuza Msumbiji na wakisimama utawasikia CCM oyee," alisema.

  Aliongeza, "Utakuta Watanzania tunaendeshwa na wafanyabiashara kati ya watano au kumi tu, ukienda kwenye sukari ni haohao, walioua viwanda ni haohao, nawahakikishia nitalala nao mbele hadi mwisho," alisema.

  Alisema kwa sasa kila Serikali inapojitahidi kufanya mambo ya maendeleo kuna watu wanataka kukwamisha, lakini kamwe hawatashinda. Alisema biashara ya sukari ni kama dawa ya kulevya, kuna kikundi cha watu ndiyo wanafanya biashara hii, wanakaa wanapanga leo tunatoa kiasi fulani leo hatutoi na wamekuwa wakienda Brazil kuchukua sukari iliyomaliza muda wake na kuileta nchini.

  "Wanakwenda kuchukua sukari ambayo imekaribia kumaliza muda wanaileta wanawauzia Watanzania, ndiyo sababu nasema wafanyabiashara wa aina hii nitapambana nao, wawe CCM, wawe Chadema, kwangu mimi ni mkong'oto tu," alisema.

  *Mbinu mbadala*

  Rais alisema kutokana na hali ya biashara ya sukari sasa, ndiyo sababu anashauri wakurugenzi wa mifuko ya hifadhi ya jamii, kufanya biashara ya sukari ambayo ni ya faida kubwa na faida ya haraka.

  "Njooni muombe vibali na kwenda kununua sukari na tutawapa ili kuja kuuza kwa Watanzania wakiwamo wanachama wenu. Alisema sukari inaweza kununuliwa nje kwa bei nzuri na inaweza kuja kuuzwa hapa nchini hadi kwa Sh800 kwa kilo, tena sukari ambayo ni bora.

  Source: Mwananchi

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku