• Breaking News

  May 21, 2016

  Serena Hotel na Ubaguzi wa Rangi!, Kwa Mzungu It is OK, Kwa Mswahili Hapana!

  Niko hapa hoteli ya Serena kwenye garden yao huku nyuma karibu na pool, niko na jamaa zangu na mgeni wangu kafikia hapa. Meza ya jirani yangu kuna wazungu nao wamekaa wanapata vivywaji.

  Wenzangu wazungu wako na kamera zao wanapiga picha kwenye mandari ya Serena, kiukweli huku kwa nyuma wana garden nzuri, yenye mandari nzuri sana!.

  Kuona hivyo na mgeni wangu si na yeye akataka picha, nikatoa kamera na mimi nimtwange picha, mara ghafla akaja mlinzi wa KK security na meneja fulani sio ndio mejeja ulinzi, akatuzuia kupiga picha!, eti watu hawaruhusiwi kupiga picha bila kibali!.

  Nikamuonyesha wale wazungu nikasema mbona wale wamepiga picha bila kuulizwa chochote au kuzuiwa, kwa nini sisi tuzuiwe?!.

  Jamaa akajibu, hao wazungu ni wageni wetu!, mwenyeji wangu mswahili akasema hata mimi ni mgeni hapa!. Jamaa kauliza number ya chumba, kaonyeshwa, akasema basi lazima mgeni huyo atoe taarifa kwa uongozi kuwa anataka kupiga picha kwenye mandari ya Serena!, ati watu wanaruhusiwa kupiga picha mandari ya Serena ni wageni wao wazungu tuu!, na waswahili labda wakiwa ni maharusi tuu!.

  Wajameni huu sio ubaguzi wa rangi mbaya kabisa wa racial discrimination ndani ya nchi yetu!, kibaya zaidi ubaguzi huu unafanywa na waswahili wenzetu, ile kuajiriwa Serena, wamegeuka vibaraka kuwaona wazungu ndio bora wanaostahili kuchukua picha lakini sisi Waswahili inakuwa nongwa!.

  Kama ubaguzi wenyewe ndio huu kwa sisi wageni tuu, hao wafanyakazi Waswahili watakuwa na hali gani humo ndani?.

  Jee tuwashitaki hawa jamaa kwa Magufuli awatimulie mbali, huwezi kuja nchi ya watu, hata kama ndio kwa kisingizio cha uwekezaji, uwekezaji gani huu wa kuwabagua wageni kwa rangi zao?!.

  NB. Kunatokeaga mbwa wa mzungu kuwa mkali hata kuliko mwenye mbwa!, isije ikawa hawa wafanyakazi Waswahili ni vijibwa tuu vya mzungu, na huo ubaguzi sio sera ya uongozi wa Serena bali wao katika kujiona bora zaidi na kujikomba komba, ndio walioinitiate huo ubaguzi ili kujionyesha tuu wao ni watu muhimu, mzungu ndio apige picha freely, Mswahili lazima uombe kibali!, na wote ni wageni wenye hadhi sawa!.

  Nashauri hii Serena imulikwe, ikithibitika ni kweli kuna ubaguzi, hili nalo ni jipu, linahitaji kutumbuliwa!.

  Kiukweli nilikasirika, na mgeni wangu amekasirika atauona uongozi kupeleka malalamiko yake ya kubaguliwa!.

  Say no to any form of discrimination!.

  Pasco

  3 comments:

  1. Huyo mlinzi zero brain kbs mgeni haangaliwi mweupe au mweusi kama ni ghalama wote wanalipa sawa kitegemea na uwezo wa mteja aondoshe fikra za kizaman

   ReplyDelete
  2. hii ni ichukulie kwa umakini zaidi !!!!sio nzuri hata kidogo.

   ReplyDelete
  3. Mtu mweusi akitwa ziro brain asichukie, sasa hao warinzi nadhani ni ziro brain, sasa mbona wageni wote wanalipa sawa, kama hakuna usawa? Mtu mweupe angelipa garama kubwa na mtu mweusi mwafrica garama ndogo hapo ingekuwa sawa

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku