Mmiliki wa klabu ya TP Mazembe Moses Katumbi anatarajiwa kufika mbele ya mahakama kujibu mashtaka yanayaomkabili ya kuwaajiri mamluki kutoka mataifa ya nje.

Katumbi alitangaza kugombea urais kwenye uchaguzi ujao katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mawakili wa Moise Katumbi wamesema Gavana huyo wa zamani wa jimbo la Katanga lenye utajiri mkubwa wa madini alikabidhiwa barua ya kufika mahakamani mwishoni mwa juma na anatakiwa kufika mbele ya mwendesha mashtaka nchini siku ya Jumatatu. Nyumba yake ilisakwa na walinzi wa serikali siku ya Jumamosi, Katumbi amekana mashtaka na ameishutumu serikali kwa kutumia njia za kumchafulia jina.

Ubalozi wa Marekani mjini Kinshasa pia umetilia shaka tuhuma hizo zinazomkabili Moses Katumbi ni zakumchafua. Rais Joseph Kabila ambaye yupo madarakani tangu mwaka 2001 bado hajabainisha iwapo atajiuzulu mwaka huu kama inavyo takiwa kwenye katiba ya nchi.

Source: BBC


Post a Comment

 
Top