May 7, 2016

Sukari Kufichwa Mbagala na Tabata ni Kukosa uzalendo

Nimekuwa nafuatilia mawazo ya watu wengi wanaojiona kuwa wao ndio wanajua uchumi kuliko wengine...Mara nyingi tunapotafuta solution ya tatizo huwa kuna short term solution na long term solution ili lisijirudie.

Sipingani na theory mbali mbali za uchumi za namna ya kusimamia uwepo wa bidhaa na mahitaji yake ila ninachopingana Nacho ni kuwa watanzania au sijui niseme waafrika wengi hatuna uzalendo wala hatuna mapenzi na nchi zetu au hata watu walio tuzunguka au sijui niseme ni uwezo mdogo wa kuelewa????

Iweje mtu afiche tani kwa maelfu store eti amehifadhi wakati hiyo bidhaa haipo Sokoni? Anatumia kifungu gani cha uchumi?

Pia nimeona hapa wanauchumi wengi wanaochangia hili suala ni wale walio kariri theory za kujibia mtihami...Mara nyingine katika application mambo sio rahisi hivyo. Lazima ujue unatatizo gani na linahitajika solution ya haraka kiasi gani ndio...ujue strategies gani utumie....

Jamani tuacheni ushabiki tuwe na mapenzi na nchi yetu na tuwe wazalendo. Hao wanao ficha sukari hawana tofauti na wahujumu uchumi....

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR