• Breaking News

  May 9, 2016

  SUMATRA yatangaza nauli kwa mabasi yaendayo kasi

  Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA imetangaza rasmi viwango vya nauli ya mabasi yaendayo kasi Jijini Dar es salaam huku ikitoa leseni kwa kampuni itakayosimamia mabasi hayo.

  Akitangaza nauli hizo mpya kwa umma, jijini Dar es Salaam leo Mei 9.2016, Mkurugenzi wa SUMATRA, Bw. Giliadi Ngewe amebainisha kuwa baada ya kupokea maombi na kisha kuyafanyia kazi wamekuja na kiwango hicho cha nauli kutokana na njia zilizopo kwenye barabara za mabasi hayo yaendayo haraka.

  Ambapo katika njia hizo kutakuwa na aina Zaidi ya mbili ambazo zitakuwa na tofauti ya ulipaji wake ikiwemo ile ndefu ambayo ni (Trunk route) huku ile ndogo itakuwa ni (Feeder route ) ama (Trunk+Feeder route).

  Kwa upande wa njia ya FEEDER kwa njia fupi ni kwa abiria wanaotoka Mbezi Mwisho kwenda Kimara ambapo nauli itakuwa ni Tsh. 400 kwa mtu mzima na Wanafunzi itakuwa ni Tsh. 200. Hii ni hivyo hivyo kutoka Kimara kwenda Mbezi mwisho.

  Kwa upande wa njia TRUNK- nauli itakuwa ni Tsh. 650 ni ile inayozihusisha njia za:

  Kimara-Kivukoni/Kivukoni Kimara

  Kimara-Kariakoo/Kariakoo-Kimara

  Kimara –Morocco/Moroco-Kimara

  Moroko-Kivukoni/Kivukoni-Morocco

  Morocco-Kariakoo/Kariakoo-Morocco

  Kariakoo-Kivukoni/Kivukoni-Kariakoo

  Kwa upande wa njia za FEEDER+ TRUNK- Nauli kwa njia hizi itakuwa ni TSH. 800 ni ile inayozihusisha njia za:

  Mbezi Mwisho-Kimara-Kivukoni/Kivukoni-Kimara-MbeziMwisho

  Mbezi Mwisho-Kimara-Kariakoo/Kariakoo-Kimara -Mbezi Mwisho

  Mbezi Mwisho-Kimara-Morocco/Morocco-Kimara-Mbezi Mwisho

  Aidha, katika tukio hilo, Mkurugenzi wa SUMATRA, Bw. Giliadi Ngewe alikabidhi leseni maalum kwa Mkurugenzi Mkuu wa UDA-RT, Bw. David Mgwassa ambapo alimtaka afanye kazi kwa mujibu wa sharia huku leseni hiyo ikiwa ni ya mwaka mmoja ambapo itaisha mpaka Mei 8 2017, Hata hivyo alieleza kuwa, UDA wanayo haki ya kuongeza mkataba kadri watakavyoona inafaa.

  Aidha, Mabasi hayo siku ya kesho Mei 10 na 11, watatoa ofa ya bure kwa kwa wananchi wote kupanda bure ilikupata elimu elekezi na namna ya uendeshaji. Hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kuyapanda mabasi hayo kama taratibu zitakazowekwa.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku