• Breaking News

  May 13, 2016

  Swali kwa CHADEMA: Edward Lowassa Aliwaeleza Nini Hadi Mkamkubali Ajiunge Chamani?

  Lowassa sasa yuko CHADEMA. Ni mwanachama halali. Lowassa amehamia huko akitokea CCM yetu. Iliripotiwa kuwa Lowassa alijieleza mbele ya Kamati Kuu ya CHADEMA kiasi cha kukubaliwa kujiunga nao na baadaye kuwa mgombea wao wa Urais mwaka jana.

  Ilielezwa kuwa Lowassa alijieleza vya kutosha juu ya makandokando yake ya ufisadi anaoshutumiwa nao. Ikasemwa kuwa Lowassa alijieleza kwa hatua kuhusu kashfa anazohusishwa nazo,ikiwemo kashfa ya Richmond. Hatimaye akakubaliwa. Akajiunga nao.

  Sasa maswali,Lowassa alieleza nini hasa? Alimtaja nani? Alisema kwanini hutajwa yeye? Mlithibitishaje maelezo yake,yaani ukweli wa alichokisema?

  Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Iringa)

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku