• Breaking News

  May 30, 2016

  Tafadhali Mama Makinda Mpe Somo Kijana Wako Naibu Spika

  Mama najua umeamua kustaafu siasa za nyumbani kwako ukiwa bado una nguvu ya kutosha lakini bado mchango wako unahitajika sana hasa kwa ustawi wa masuala mazima ya bunge, kiti cha sasa kinapwaya zaidi awapo Mwanamke mwezio, mchango wako mama unaweza kujenga zaidi, wewe ni mfano wa kuigwa katika weledi wa kuendesha bunge na umeacha pengo ambalo linaonekakana gumu kuzibika.


  Tafadhali mama yangu mwite kijana wako mwanamke na mwanachama mwezio mpe darasa mambo yanamwndea Kombo, mwelekeze namna ya kua mvumilivu kama kiongozi anayeweza kua na uwezo wa kutumia mizani vizuri awapo katika kiti chake.Sipendi sana kuona mwanamama akilalamikiwa sana kwa utendaji wake, mfunde namna ya kuchuja hoja zenye maslahi ya kitaifa na zisizokua na maslahi ya kitaifa, mfunde namna ya kusikiliza hata kama anona ni pumba maana kila mtu anayo haki ya kutoa hoja na kusikilizwa, mwele atambue kua anaongoza kila aina ya kichwa na asili yake.Mwambie ifike mahali apime upepo kulingana na aina ya tukio linalotolewa hoja,Mfunde namna ya kutafuta suluhu kwa mazungumzo na maridhiano kama ulivyokua ukifanya wewe maana ubabe hua una kikoma.


  Ni rai yangu kua wewe kama malkia wangu wa nguvu utatumia busara na hekina zako kuweka baadhi ya mambo sawa pindi unapoona hayaendi sawa ikikubidi. Najua kaka yangu Ndungai anao uwezo huo lakini naona pengine darasa lake bado halijamkolea kijana huyu mwanamama maana naamini pia kwa Ndungai kuna kitu ulimwachia kwa muda wote ulipokua pamoja nae.

  By Mahanju

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku