• Breaking News

  May 8, 2016

  TAKUKURU yamnasa aliyeficha sukari tani elfu 4579

  Msemaji wa TAKUKURU Tunu Mleli, amesema wanamshikilia mfanyabiashara huyo ili aweze kujibu tuhuma hizo za kuficha sukari jambo ambalo ni kinyume na sheria za biashara na pia bado taasisi hiyo inaendelea na upelelezi katika maeneo mengine.

  Bi. Tunu ameongeza kuwa kitendo cha wafanya biashara kuficha sukari ni uhujumu uchumi hivyo wote watakaopatiokana watachukuliwa hatua za kisheria.

  Sukari katika maeneo mengi nchini imeadimika huku bei ikiwa ni tofauti kwa maeneo mengi ambapo maeneo mengi imependa hadi kufikia kilo 3500 kutoka shilingi 2000 huku wafanya biashara wadogo wakipanga foleni katika maeneo mbalimbali ili kuweza kupata sukari ya kuwauzia wananchi.
  Kufuatia tatizo hilo serikali imeamua kuagiza sukari kutoka nje ya nchi ili kuweza kuhakikisha wananchi hawapati taabu zaidi, ikiwa inasubiriwa ikagundulika kwamba wafanyabiashara wengi wameficha sukari kwa lengo la kuuza kwa bei ya juu ikishaadimika zaidi hasa mfungo wa mwezi Raadhani.

  Hivi karibuni jeshi la polisi mkoani Singida liliwashikilia wafanyabiashara wawili kwa kuficha sukari mifuko 665, ambapo kwa taarifa zinazozidi kupatikana katika maeneo mbalimbali ya nchi wafanyabiashara wengi wameficha sukari.

  Kwa nyakati tofauti Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameweka wazi kwamba wafanyabiashara ambao wameficha sukari hawana lengo jema na serikali yake haitawavumilia.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku