Mmiliki wa baa maarufu ya Macheni iliyopo Magomeni jijini Dar es
Salaam, Hussein Macheni amefariki dunia leo baada ya kuanguka ghafla akiwa
nyumbani kwake Magomeni.

Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu ni kwamba Macheni alianguka ghafla majira ya
saa 3 asubuhi na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo iligundulika kuwa
tayari amefariki.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Muhimbili kusubiri taratibu nyingine. Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. AMEN.


Post a Comment

 
Top