• Breaking News

  May 17, 2016

  TFDA yateketeza bidhaa za mamilioni

   Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania(TFDA) Kanda ya Ziwa, imeteketeza bidhaa  feki zenye thamani ya zaidi ya Sh171 milioni zilizokamatwa wakati wa operesheni iliyofanyika Januari hadi Mei, mwaka huu.

  Baadhi ya bidhaa zikiwamo za vyakula, vipodozi na dawa zilizokamatwa kwenye maduka mbalimbali jjijini Mwanza hazikuwa na usajili au uthibitisho kutoka TFDA.

  Mkaguzi wa chakula wa mamlaka hiyo, Julius Panga amesema baadhi ya bidhaa zilikutwa zimeisha muda wa matumizi huku nyingine zikiwa zimehifadhiwa eneo lisilofaa kulingana na kanuni za afya.

  Panga ametaja bidhaa zilizokamatwa na kuteketezwa kuwa ni maziwa ya kopo, dawa za binadamu, pombe kali, biskuti, vipodozi na juisi.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku