• Breaking News

  May 23, 2016

  TUHUMA: Ubadhirifu mkubwa wa ruzuku CHADEMA waripotiwa

  Na Chotipembe Ntuguja.

  Matumizi ya fedha za ruzuku ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yaimeibua maswali mengi miongoni mwa watendaji wakuu wa chama hicho.

  Chanzo chetu cha habari ndani ya CHADEMA kimedokeza kuwa kumekuwa na uhamisho mkubwa wa fedha mara tu ruzuku inapoingi kwenye akaunti. Zaidi ya shilingi milioni mia mbili zimekuwa zikihamishwa kila mwezi kwa madai kukijenga chama ila jambo la kustaajabisha ni kuwa pesa hizo huamishiwa kwenye akaunti mpya zilizofunguliwa katika benki moja ya biashara kisha kutolewa taslimu.

  Kwa masikitiko makubwa mtoa taarifa huyu alisema ‘kaka ninachokuambia kwa sasa pamoja na ruzuku kuongezeka lakini nakuapia chama hakitafanya maendeleo muhimu kama ya kujenga ofisi wala kuimarisha ofisi za kanda na majimbo, kwa sasa hali ni mbaya tokea Dr. Slaa ameondoka mambo yamekuwa hovyo, taratibu za ofisi hazifuatwi na kumekuwa na matumizi holela ya fedha kwa mambo yasiyo na msingi’’.

  Chanzo kingine kilitudokeza kuwa ‘pesa zinazohamishwa baada ya kutolewa benki taslimu ni malipo kwa mwanasiasa mkongwe aliyehama kutoka CCM na Kuja CHADEMA kwa mujibu wa makubaliano’’, ameendelea ndugu yangu mwenyekiti amekuwa ‘mbogo’ hataki kuulizwa kuhusu suala hili na ametamka yeyote atakayeendeleza mjadala atatimuliwa’’.

  ‘Mimi na vijana wenzangu tuliacha kazi, nilikuwa afisa wa serikali nikajitosa kugombea ubunge Mkoa wa mbeya nilitumia pesa zangu zote mbona silipwi? sababu kura nilizo pata zimesaidia kuongeza ruzuku japo nilikosa ubunge’

  Aidha katika hatua nyingine kumekuwa na matumizi makubwa katika mikutano ya chadema huku ikiambatana na hafla kubwa kwenye mahoteli makubwa baada ya mikutano, ndugu yangu mkutano wa juzi pale Mwanza Gold Crest chama kililipa zaidi ya milioni mia mbili hamsini kwa ajili ya vyakula na vinywaji kwa siku mbili ukiachilia mbali posho za wajumbe’’ alidokeza mtoa habari wetu ndani ya chama. Wanatuhumiwa baadhi ya vigogo kuungana na watoa huduma kupandisha gharama ili kujinufaisha ‘ten percent’.

  Malalamiko mengine yamejikita kwenye ubaguzi wa dhahiri kwa baadhi ya viongozi ambao hawakuunga mkono suala la mwenyekiti kuwapa ujumbe wa kamati kuu waliokuwa mawaziri wakuu wa awamu ya tatu na nne, Fredrick Sumaye na Edward Lowassa.

  ‘Ndugu yangu sasa hivi mwenyekiti hana maamuzi na baadhi ya viongozi wameshaambiwa wasichukuwe fomu kugombea nyadhifa kwenye uchaguzi ndani ya chama unaotarajiwa kufanyika mwaka 2018.

  ‘Ninachokwambia baadhi ya viongozi wapo sababu ni wabunge lakini kulekea uchaguzi mkuu 2020 mtasikia mengi, kuna fukuto kubwa sana na mwenyekiti kwa sasa amefanya shingo ngumu’’

  Baada ya mazunguzo haya mwandishi alimtafuta Mwenyekiti wa Taifa ambaye alipokea simu baada ya kuombwa miadi alijibu ‘I am busy’ yaani kabanwa na shughuli, mara ya pili alivyoulizwa tuhuma hizi alimwambia mwandishi aende kwa katibu mkuu ambaye alisema ‘no comment’’ baadaye akajibu anashughuli nyingi ikiwamo safari ya nje ya nchi hivyo hakusema zaidi.

  Maswali yangu kutokana na habari hii.

  Je ni nani wanalipwa mamilioni haya?

  Ni makubaliano gani ya siri baina ya uongozi na watu bila ya maamuzi ya vikao?

  Je waliokosa ubunge nao wanalipwa fidia hii?

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku